Family Church (uk. 14) liliazimia kuwaandaa washiriki kugeuza maingiliano ya kila siku kuwa mazungumzo ya Injili. Zana ya Duara 3 waliyoiunda ilichangia kuongeza mara tatu idadi ya waliobatizwa kutoka 80 mwaka 2013 hadi 240 mwaka 2014. Harakati katika sehemu kadhaa za ulimwengu zimeirekebisha zana ya Duara 3.
Jimmy Scroggins anapitia Duara 3 ya asili kwa dakika sita katika namb.net/video/3circlesguide.
Southern Baptist North American Mission Board liliigeuza kuwa programu ya simu janja: “Life Conversation Guide.”
Maboresho ya ziada yaliyo hapa chini yalitokana na matumizi ya Duara 3 katika kutafuta Nyumba ya Amani katika mabara mawili.
Malachi mwenye umri wa miaka kumi anaonyesha marekebisho yaliyo hapa chini katika video hii ya dakika nne: vimeo.com/128678770
MBINU YA MAZUNGUMZO
Utafiti mmoja unaonyesha kwamba Wamarekani wana wastani wa mazungumzo 27 kwa siku. Mara nyingi haya huibua mapambano au masuala yanayotualika kutoa sababu ya tumaini tulilo nalo (1 Petro 3:15).
Duara 3 ni zaidi ya wasilisho rahisi la Injili, ni mbinu shirikishi ya:
- kuongoza mazungumzo ili yajumuishe Injili
- kusimulia habari ya Mungu ndani ya habari yako mwenyewe
- kualika mwitikio
- kuwafunza waamini wapya kufanya vivyo hivyo.
MFANO WA MAZUNGUMZO
Hebu tujiunge na Chris na Larry katikati ya mazungumzo, Larry anapotaja jambo lililomkatisha tamaa.
L“Imekuwa siku ngumu, ikianza na ugomvi na mke wangu.”
C“Ndiyo, nimekuwa na siku kama hizo. Rafiki mzuri alinishirikisha jambo lililonipa tumaini na kunisaidia kubadilika. Wewe ni rafiki mzuri, na ningependa kukushirikisha.”
C anachora duara na kuandika Uvunjifu ndani yake: “Tunaishi katika ulimwengu wa uvunjifu, uliojaa watu wanaoumia wakiumizana. Zamani nilikuwa nimejaa hasira kiasi kwamba niliimwaga kwa wale walio karibu nami. Niliweza kujiona nikifanya hivyo, lakini sikujua jinsi ya kuacha.”

C anachora mishale iliyopindapinda ikitoka na kujirudia kwenye Uvunjifu: “Tunajaribu kuukimbia uvunjifu katika mahusiano, kazi, starehe au kwa kupunguza maumivu yetu, lakini hili linaleta tu uvunjifu mkubwa zaidi. Zamani nililewa mara kwa mara, na nilikuwa na msururu mrefu wa mahusiano. Lakini mwishowe nilihisi tu maumivu zaidi.”
L“Ndiyo, naelewa unachomaanisha. Nimejikita katika kazi yangu, lakini inaonekana inaisambaratisha ndoa yangu. Kwa hiyo ulijifunza nini?”
C anachora duara la pili, upande wa kushoto wa lile la kwanza, na kuandika Mpango wa Mungu ndani yake. “Nilijifunza kwamba uvunjifu wetu haukuwa mpango wa asili wa Mungu! Tunaona ushahidi wa mpango Wake tunapoona uzuri wa mtoto mchanga aliyezaliwa au mapambazuko au machweo ya ajabu.”
C anachora mshale kutoka Mpango wa Mungu hadi Uvunjifu na kuandika dhambi juu yake. “Lakini kila mmoja wetu amemwasi Mungu na kuuacha mpango Wake. Biblia inaita hili dhambi, na hili linatuacha katika uvunjifu.”
C anachora duara la tatu chini na katikati ya yale mawili ya kwanza (likiunda pembetatu iliyopinduliwa ya duara), na kuandika Yesu ndani ya nusu ya juu. “Mungu aliona kwamba hatungeweza kuukimbia uvunjifu wetu sisi wenyewe, kwa hiyo Mungu alidhihirisha upendo wake kwetu!”
C anachora mshale unaoelekea chini chini ya jina la Yesu ndani ya duara. “Alimtuma Yesu duniani na Yesu aliishi maisha makamilifu.”
C anachora msalaba kando ya mshale unaoelekea chini. “Aliteseka kifo cha kutisha msalabani ili kuuchukua uvunjifu wetu juu Yake.”
C anachora mshale unaoelekea juu kando ya msalaba. “Kisha Yesu alifufuka tena. Ana nguvu juu ya mauti! Yu hai!”
C anachora mstari kutoka Uvunjifu hadi Yesu, anauwekea alama ya taji la mfalme, na kuandika kurejeshwa. “Yesu alisema ukigeuka kutoka katika uvunjifu wako, ukiamini kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, na kumkiri Yesu kama mfalme wa maisha yako, utarejeshwa kwenye mpango wa Mungu! KWA HIYO NILIFANYA HIVYO! Na sasa…”
C anachora mstari kutoka Yesu hadi Mpango wa Mungu na kuuwekea alama kukua. “Ninakua katika mpango wa Mungu …”
C anachora mshale kutoka Mpango wa Mungu kurudi kwenye uvunjifu. “Na ninakwenda kuwaeleza wengine walio katika uvunjifu kuhusu HABARI HII NJEMA!”
L“Hiyo ina nguvu sana!”
C“Unajiona wapi katika picha hii?”
L anaonyesha Uvunjifu.
C“Na ungependa kuwa wapi?”
L“Katika mpango wa Mungu.”
C“Unaweza kufika huko sasa hivi. Larry, unaamini kwamba Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu?”
L“Ndiyo.”
C“Larry, unataka kugeuka sasa kutoka katika uvunjifu wako?”
L“Ndiyo.”
C“Je, utamkiri Yesu, si mimi, kwamba unachagua kumfuata Yeye kama mfalme wako? Mwambie tu hivyo!”
L“Sawa. Yesu, ninageuka kutoka katika uvunjifu wangu na ninachagua kukufuata. Uwe mfalme wa maisha yangu, Yesu!”
C“Hongera sana Larry! Sasa hebu nikuonyeshe mistari kadhaa katika Biblia!”
C anafungua Mathayo 28:18. “Yesu alisema, ‘nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.’ Unaamini kwamba Yesu ana mamlaka yote mbinguni na duniani?”
L“Ndiyo.”
C“Unampa Yesu mamlaka juu ya maisha yako?”
L“Ndiyo.”
C“‘Basi nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi.” Larry, unajua ‘mwanafunzi’ ni nini?”
L“Hapana,”
C“Ni kama mwanagenzi, anayemfuata Yesu na kufanana Naye! Unataka kuwa mwanafunzi wa Yesu?”
L“Ndiyo, lakini sijui jinsi gani.”
C“Tutakutunza na kukusaidia! Yesu aliendelea, ‘mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.’ Ubatizo ni ishara ya kile Yesu alichotufanyia—Alikufa, akazikwa, na siku tatu baadaye akafufuka kutoka kwa wafu! Ubatizo pia ni picha ya muujiza unaotokea ndani yetu tunapomfuata—tunaufia utu wetu wa zamani na tunafufuliwa ili kutembea maisha mapya pamoja na Yesu! Je, utautii mfano na agizo la Yesu la kubatizwa sasa?”
L“Ndiyo, tufanye hivyo!”
C“Vizuri sana. Sasa hebu niendelee, ‘mkiwafundisha kuyatii yote niliyowaamuru ninyi.’ Larry, tunaweza kurudi na kuendelea kukufundisha jinsi ya kuyatii yote ambayo Yesu aliamuru?”
L“Bila shaka. Lini?”
C“Vipi wakati huu huu wiki ijayo?”
L“Vizuri sana!”
C“Tazama sehemu hii ya mwisho, Larry. Yesu aliahidi, ‘Na hakika mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata mwisho wa nyakati.’ Larry, hilo linakufanya ujisikie vipi?”
L“Vizuri Sana. Vizuri Sana.”
C“Usisahau kamwe ahadi ya Yesu kwako, Larry! Sasa twende tukatafute maji ili uweze kulitii agizo la Yesu na kubatizwa!”
L“Twende!”
Ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika Mission Frontiers 38:2 (Mac./Apr. 2016), uk. 33-35. Frontier Ventures. Imeshirikishwa kwa ruhusa.


